Rais wa
Marekani Barack Obama anasubiriwa mapema leo asubihi jijini Varsovie
kwa ajili ya kujaribu kuuhakikishia washirika wake wa Ulaya kuhusu
hofu iliopo juu ya mzozo wa Ulaya ya mashariki na mwenendo wa
serikali ya Moscou nchini Ukraine wakati huu mapigano makali
yakiripotiwa kati ya wanajeshi wa serikali na wakereketwa wanaodai
mjitengo.
Rais Obama
ambaye ameondoka jijini Washington jana jioni atashiriki katika
sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya uchaguzi wa kwanza kidemokrasia
nchini Pologne iliokuwa zamani katika muungano wa kisovieti.
Ben Rhodes
naibu mshauri wa rais Obama anayehusika na maswala ya Usalama
amesema, Rais Obama atatumia fursa ya ziara yake hiyo barani Ulaya
kusisitiza juu ya ushirikiano kati ya Marekani na Umoja wa ulaya kwa
ajili ya Usalama katika bara la Ulaya ya mashariki kulinda
demokrasia.
Watakuwepo
pia jijini Varsovie ma rais francois Hollande wa Marekani, Knasela wa
ujerumani Angela Merkel na Joachim Gauck pamoja na viongozi kadhaa wa
kisiasa barani Ulaya ya kati na ya kaskazini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire