Ujumbe wa
Umoja wa Mataifa nchini DRCongo Munusco umesema unataka kuandaa
mazingira mazuri kuhakikisha waasi wa kihutu waliopiga kambi nchini
Congo wanajisalimisha na silaha zao kwa idadi kubwa zaidi ya
ilionekana juma lililopita mashariki mwa DRCongo.
Jenerali
Abdallah Wafi naibu kiongozi wa Monusco amesema watato mchango wa
vifaa, usalama, wanajeshi, chakula na hata madawa kuhakikisha
mchakato huo unafikia malengo yake.
Kwa mujibu
wa kiongozi huyo, Monusco kwa sasa inatia kipao mbele kuhakikisha
mpango huo unafana baada ya kushindikana mara kadhaa kufuatia
mazingira mabaya ya kuwakusanya waasi hao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire