Mjumbe
maalum wa nchi ya Marekani katika ukanda wa maziwa makuu Russ
Feingold anaelezea wasiwasi wake kufwatia kesi inayoendeshwa nchini
Burundi dhidi ya mwanaharakati Pierre Claver Mbinimpa aliyeko
kizuwizini.
Katika
mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa, mjumbe huyo ameiomba
serikali ya Burundi kuzingatia taratibu za kisheria katika kuendesha
kesi hiyo ya Mbonimpa ambaye anatuhumiwa kuhatarisha usalama kwa
madai yake kuwa vijana Imbonerakure wanapewa mafunzo ya kijeshi
mashariki mwa DRC, jambo ambalo serikali ya Bujumbura inapinga.
Kwa mara
nyingine tena, Mbonimpa amefikishwa jana kizimbani kujibu mashtaka
hayo, huku mamia ya wanaharakati, pamoja na mabalozi na waandishi wa
habari wakishuhudia tukio hilo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire