Russ Feingold |
Ma balozi
kadhaa waandamizi wanaohusika na ukanda wa maziwa makuu wametowa
shutma katika taarifa yao ya pamoja iliotolewa jana kuhusu kuminywa
kwa harakati za upinzani na uhuru wa kujitetea nchini Burundi wakati
huu taifa hilo likielekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais uliopangwa
kufanyika mwakani.
Merry Robinson |
Mjumbe
maalum wa Umoja wa Mataifa Mary Robinson, muakilishi wa Umoja wa
Afrika Boubakar Diarra, mratibu wa shughuli za Umoja wa Ulaya Koen
Vervaeke pamoja na mjumbe maalum wa Marekani
Russ Feingold wamekutana mwishoni mwa juma lililopita na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Katika
taarifa yao ya pamoja wajumbe hao wamesema kutiwa wasiwasi sana na
hali iliopo nchini Burundi ambapo nafasi za kisiasa na uhuru wa raia
na kuzuia kwa shughuli za upinzani, mashirika ya kiraia na vyombo
vya habari, wakati huu nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu 2015
".
Martin Kobler |
Ma balozi
hao wameshtumu pia hatuwa zinazo vuruga mchakato wa uchaguzi hatuwa
inayoweza kuzuia ushiriki wa wadau wote, hali ambayo inayoweza
kurudisha nyuma hatuwa zilizofikiwa katika kuponya donda la maumivu
yaliolikumba katika miaka ya hivi karibuni.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire