Pages

mardi 3 juin 2014

MASHIRIKA YA KIRAIA NCHINI BURUNDI YATAKA UCHUNGUZI UFANYIKE KUHUSU TAARIFA ZA UGAVI WA SILAHA KWA VIJANA WA CHAMA TAWALA

Vijana wa Imbenerakure katika moja ya sherehe zao

Miezi miwili baada ya kuvuja kwa taarifa kutoka Umoja wa Mataifa kuhusu uwepo wa shughuli za ugavi wa silaha kwa vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD nchini Burundi Imbonerakure, hatuwa iliopelekea kufukuzwa nchini humo kwa mwanadiplomasia wa Umoja huo na ambayo imekuwa sababu ya kutiwa nguvuni kwa mwanaharakati wa haki za binadamu na mtetezi wa haki za wafungwa Pieere Claver Mbonimpa, mashrika ya kiraia nchini humo yameomba uchunguzi ufanyike kuhusu taarifa hii.

Muungano wa mashirika ya kiraia nchini humo umesaini waraka kwa raia wa Burundi Pierre Nkurunziza na kwa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kufanyika kwa uchunguzi kuhusu taarifa hii.
Vital Nshimirimana mwenyekiti wa mashirika ya kiraia FORSC

Mratibu wa shughuli kwenye muungano wa mashirika ya kiraia Vital Nshimirimana amesema lengo hasa ni kutaka kujuwa ukweli kuhusu taarifa hii kwani serikali ya burundi haitaki kufanyika kwa uchunguzi ili kutowa mwanga zaidi kuhusu taarifa za vijana wa chama tawala wanaopewa mafunzo ya kijeshi katika ardhi ya Congo.

Lengo hasa la waraka huu ni kuhakikisha zinakusanywa ma elfu ya sahihi kwa kipindi cha majuma mawili kuishinikiza serikali ya burundi na jumuiya ya kimataifa kuanzisha uchunguzi kuhusu taarifa hii ya kutatanisha.

Philippe Nzobonariba

Upande wake ya Burundi imetupilia mbali harakati hizo za masharika ya kiraia nchini humo ya kupiga kampeni ili kukusanya saini kwa maelfu katika wiki mbili zijazo, kuilazimisha kuanzisha mchakato wa kuchunguza madai kwamba imegawa silaha kwa vijana wa chama tawala – Imbonerakure.

Majibu ya Serikali ya Burundi hayakuwa na kigugumizi wakati Msemaji wa Serikali ya Burundi Philippe Nzobonariba ametuhumu mashrika ya kiraia nchini humo kuendelea kuwa vibaraka wa vyama vya upinzani.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...