Pages

vendredi 6 juin 2014

OFISI YA UMOJA WA MATAIFA NCHINI BURUNDI YAITAKA SERIKALI YA NCHI HIYO KUREJELEA UAMUZI WAKE

Muakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi Onyang Anyongo
Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi imeitaka serikali ya nchi hiyo kurejelea upya uamuzi wake wa kumrejesha nyumbani mwanadiplomasia wa kitengo cha Umoja wa mataifa nchini humo aliyekuwa anahusika na maswala ya usalama kwenye ofisi hiyo baada ya kukamatwa na risase kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa jijini Bujumbura.

Serikali ya Burundi ilimpa siku ya jumanne saa 48 mwanadiplomasia Abednego Mutua raia wa Kenya kuondoka nchini humo kutokana na kitendo hicho cha kumkuta na risase wakati akijiandaa kupanda ndege kuelekea nchini Kenya.

Mutua amekuwa mwanadiplomasia wa pili wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi kufurushwa kwa kipindi cha miezi miwili. Msdemaji wa Ofisi ya umoja wa Mataifa nchini Burundi Vladimir Monteiro amesema tukio hilo la kwenye uwanja wa ndege ni la bahati mbaya kwani afisaa huyo alisahau kuondowa risase hizo za silaha yake kwenye begi lake kabla ya kuondoka, kwani mtaalamu huyo wa Usalama anaruhusiwa kubeba silaha kwa mujibu wa makubaliano ya serikali ya burundi na Umoja wa Mataifa

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inaiomba serikali ya Burundi kurejelea upya hatuwa yake hiyo


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...