Pages

mercredi 4 juin 2014

SERIKALI YA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI YAZUIA MATUMIZI YA UJUMBE MFUPI KWENYE SIM

Waziri Mkuu wa Jmhauri ya Afrika ya Kati Andre Nzapayeke
Matumizi ya ujumbe mfupi wa simu yamepigwa marufuku nchini jamhuri ya Afrika ya kati kwa ajili ya usalama nchini humo, hatuwa hiyo imechukuliwa baada ya kuwepo kwa dalili kuwa unachangia kuhamasisha machafuko nchini humo.

Hatua hiyo ya kiusalama imetangazwa jana na Wizara ya Posta na Mawasiliano na kuanza kutekelezwa hadi itakapotangazwa tena upya ili kuchangia kurejesha usalama katika nchi ambayo imegubikwa na matukio ya vurugu na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Uamuzi huo unakuja baada ya Waziri mkuu wa nchi hiyo André NZAPAYEKE kuwaandikia barua Waziri na wakurugenzi wa Posta na mawasiliano baada ya vurugu zilizojitokeza juma lililopita na baada ya wito wa mgomo uliotolewa mapema wiki hii kwa njia ya sms.
Aidha, hatua hii inakuja baada ya wito wa Waziri mkuu kuwaomba wafanyakazi wote warejee kazini kuanzia jana baada ya siku kadhaa za maandamano na kusimamishwa kwa shughuli zote za kijamii mjini Bangui.


Taarifa kutoka vyanzo vya kiserikali zimebaini kuwa matumizi ya ujumbe mfupi au sms yatasimamishwa kwa siku chache zijazo, na tayari watu wakijaribu kutuma ujumbe wa maandishi kupitia mtandao wa Orange maarufu mjini Bangui yanatokea majibu kwamba ni marufuku kuandika SMS.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...