Muakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi Balozi Onyang Nyong |
Waziri wa
mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure amesema uongozi wa uwanja wa
ndege wa kimataifa wa jijini Bujumbura ulimkuta mwanadiplomasia
Abednego Mutua raia wa Kenya na Magazine 2 zikiwa na risase 15 wakati
akijiandaa na safari, taarifa iliotolewa kwa ofisi ya Umoja wa
Mataifa kabla ya kuchukuliwa hatuwa ya kupewa muda wa saa 48 kuondoka
nchini Burundi, na hili haligusi hata kidogo uhusiano bora uliopo
kati ya serikali na Umoja wa Mataifa.
Mshauri wa
rais anaye husika na mawasiliano Willy Nyamitwe amefahamisha kuwa
mwanadiplomasia huyo alikmamatwa na silaha Mei 25 wakati akijiandaa
kwa safari kuelekea nchini Kenya.
April 17
serikali ya Burundi ilichukuwa hatuwa kama hiyo ya kumfurusha
mwanadiplomasia wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa anaye husika na maswala
ya Usalama Paul Debbie, baada ya kuvuja kwa taarifa kutoka Umoja huo
kuhusu serikali ya burundi kuwapa silaha vijana wa chama tawala cha
CNDD-FDD wa Imbonerakure.
Serikali ya
Burundi ililaani vikali taarifa hiyo iliozagaa kwenye vyombo vya
habari na kuiita kuwa ni uvumi usiokuwa na msingi na ambo unania
pekee ya kuipakatope serikali.
Hata hivyo
kiongozi mmoja wa Bnub ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema
serikali ya Burundi inataka tu kulipiza kisase baada ya kuvuja kwa
taarifa hizo, kwa sababu Mutua ni kiongozi wa Usalama ambaye
anaruhusiwa kumiliki silaha, na hakuwa tu muangalifu kwa kusafiri na
silaha.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire