Rais wa
kipindi cha mpito nchini jamhuri ya afrika ya kati Catherine Samba
Panza, amezuru jana Jumapili katika Hospitali kuu jijini Bangui
kuwajulia hali waathirika wa machafuko ya kidini yanayolikumba taifa
hilo.
Samba Panza
amejiunga na familia za waathirika hao katika kuwatolea msaada wa
fedha kwa ajili ya matibabu na maswala mengine muhimu hususan
chakula.
Rais Panza
amesema kulikuwa na umuhimu wa kuwajulia hali watu hao wanaendelea
kutaabika na hali iliowakumba, na kwamba shughuyli za upokonyaji
silaha lazima zifanyike kwa mpango zikisimamiwa na kikosi cha umoja
wa Afrika, na kikosi cha ufaransa cha operesheni Sangaris nchini humo
Misca.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire