Pages

lundi 30 juin 2014

MIAKA 54 YA UHURU WA DRCONGO


Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC hii leo wanafanya sherehe za kumbukumbu ya miaka 54 tangunchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa mkoloni mbelgiji, sherehe ambazo zinajiri wakati huu wananchi wa taifa hilo wakikabiliwa na changamoto kem kem.

Hapo jana rais Josephu Kabila alitoa hotuba kuelekea siku hii ya leo muhimu kwa wananchi wa taifa hilo ambao wameendelea kushuhudia hali ngumu ya maisha pamoja na kuzorota kwa usalama kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Kwenye hotuba yake rais Joseph Kabila amelipongeza jeshi la nchi hiyo licha ya changamoto linazokabiliana nazo lakini limekuwa imara kulinda mipaka ya nchi yake dhidi ya wavamizi.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...