Pages

jeudi 5 juin 2014

WALINDA AMANI NCHINI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI WALAUMIWA KUTEKELEZA MAUAJI

Vikosi vya kulinda amani nchini jamhuri ya Afrika ya kati vimetuhumiwa kwa mara nyingine kutekeleza vitendo vya uhalifu na ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya raia nchini humo.

Baada ya tuhuma zilizoelekezwa kwa askari wa Tchad waliolazimika kuondoka nchini humo, sasa ni askari wa Congo Brazzaville ndio wanaotuhumiwa kwa kukiuka haki za Binadamu kama ilivyoripotiwa na shirika la kimataifa la Human Rwight watch.


Ripoti hiyo inabaini kuwa watu wasiopungua 11 waliokamatwa na askari wa Congo-Brazaville tarehe 24 mwezi Mei mjini Boali kwenye umbali wa kilomita themanini na mji mkuu Bangui wametoweka na kupelekwa kusikojilikana.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...