zaidi ya
watu 100 wanaarifiwa kukwama katika vifusi vya ghorofa ilioporomoka
siku ya Jumamosi katika mji wa Chennei kusini mwa India ambapo watu
zaidi ya kumi wamepoteza maisha
Wengi wa
waliopoteza maisha ni wafanyakazi walikokuwa wakishiriki katika
shughuli za ujenzi. Kiongozi mmoja nchini India amesema takriban watu
132 bado wapo chini ya vifusi ambapo wengi wao ni kutoka katika jimbo
la Andhra Pradesh
Watu 26
pekee ndio ambao wameokolewa hadi sasa. Chanzo cha jengo hilo
kuporomoka chaelezwa kuwa ni kutokana na hali ya hewa. Polisi
imewatia nguvuni viongozi wawili wanaohusika na ujenzi wa jengo hilo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire