Umoja wa
Mataifa umesema mwishoni mwa juma kwamba unatiwa wasiwasi na
kuzuiliwa jela kwa mwanaharakati wa haki za binadamu nchini burundi, Pierre Claver Mponimba tangu Mei 15.
Kwa mujibu
wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Strephane Dujarric, Umoja wa Mataifa
unawasiwasi kuhusu mwanaharakati huyo Pierre Mbonimpa na kuitaka
serikali ya burundi kuheshimu haki ya msingi na kuruhusu kesi yake
isikilizwe huku misingi ya kimataifa ya haki za binadamu
ikiheshimiwa.
Pierre Claver Mbonimpa mwanaharakati wa haki za binadamu na za wafungwa APRODEH
anazuiliwa jela kwa kosa la uhaini.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire