Nahodha wa timu ya taifa ya Burundi Intamba Mu Rugamba Valerie Nahayo ambaye anacheza soka la kulipwa barani Ulaya, ametangaza hivi majuzi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kwamba amestafu kuchezea timu ya taifa ya Burundi baada ya kupeperusha bendera ya taifa kwa kipindi cha miaka 12.
Nahayo amesema ameridhishwa kuichezea timu ya taifa na hato jutia kamwe uamuzi wake wa kuichezea timu yake ya taifa kwa moyo mkunjufu, na kutowa shukran za dhati kwa wale wote waliomtolea sapoti kwa kipindi chote hiki akiwa nahodha wa timu hiyo. Amesema ata miss mambo mengi katika timu ya taifa na kuwatakia wachezaji wenzake kila la kheri.
Hata hivyo Twite Valerie Nahayo hakuweka bayana sababu zilizomlazimu kuchukuwa uamuzi huo, ambao ameutowa muda tu baada ya timu ya taifa Intamba Murugamba kushindwa kusonga mbele kwenye mtoano wa kuwania kufuzu kombe la mataifa bingwa barani Afrika huko Moroco mwakani.

Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire