Umoja
wa Mataifa umeonya juu yan hali inayoendelea nchini Iraq ya kusonga
mbele kwa wanamgambo wa kijihadi kuelea katika mji wa Bagdad na
kuongeza kuwa hali hiyo inatishia usalama na mustakabaliu wa nchi
hiyo.
Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa hatua ya wapiganaji
wa kijihadi kufika kwenye eneo lililoko kilometa 60 kutoka Bagdad
linaashiria kuwa Iraq imeingia katika hatua mbaya na lazima hatua
stahili zichukuliwe kudhibiti hali hiyo.
Hayo
yanajiri wakati huu Marekani ikiwa imetuma wanajeshi wapatao 275
kulinda ubalozi wa marekani mjini Bagdad na hii ni mara ya kwanza kwa
marekani kutuma wanajeshi tangu kuondoka kwa majeshi yake mwaka 2011
kufuatia uvamizi iliofanya mwaka 2003.
Marekani
kupitia kwa amiri jeshi mkuu rais Barack Obama inafikiria uwezeka wa
kufanya mashambuli ya anga kwa kutumia ndege zisizo na rubani ili
kukabiliana na wapiganaji hao ambao wameteka baadhi ya maeneo nchini
Iraq.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire