Viongozi watano wa kundi la Taliban wamewasili nchini Qatar baada ya kuachiwa huru kutoka katika jela la Guantanamo Bay katika hatuwa ya Marekani kubadilishana wafungwa na Taliban, hatuwa ambayo imezua mtafaruku.
Wafungwa hao
wa Taliban walisafirishwa kwa ndege ya kijeshi ya Marekani C-17
katika eneo la huba jana jumapili. Viongozi hao wa Taliban ni pamoja
na Mohammad Fazl, le mollah Norullah Noori, Mohammed Nabi, Khairullah
Khairkhwa na Abdul Haq Wasiq.
Kiongozi
mkuu wa Taliban aliyeachiwa huru Mollah Omar amepongexza hatuwa hiyo
na kusema kuwa ni ushiondi mkubwa kwa kundi hilo.
Kufuatia
hatua hiyo umeibuka wasiwas juu ya usalama baada ya kuachiwa kwa
viongozi wandamizi wa Taliban lakini Rais wa Marekani Barack Obama
anaona kuwa Marekani itabaki kuwa salama hata baada ya kuachiwa kwa
wafungwa hao wa Taliban.
Kwa upande
wake waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amesema kuwa walichukua
hatua hiyo ili kumrejesha mwanajeshi Bowe Bergdahl lakini hadhani
kama hatua inaweza kutishia usalama wa marekani.
Aidha Chuck
Hagel amekanusha kuwa taarifa kuwa serikali yake imefanya makubaliano
na magaidi na kuongeza kusema kuwa hatua hiyo ni ya kawaida katika
utaratibu wa kuachiwa kwa wafungwa kivita.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire