Pages

mercredi 2 juillet 2014

MAWAZIRI WA NCHI 11 ZA UKANDA WA AFRIKA MAGHARIBI WAKUTANA KUJADILI KUHUSU MARADHI YA EBOLA



Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwenye nchi za Afrika Magharibi imefikia watu 467 na kuonya kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka.

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo uliozikumba nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone, WHO inasema kuwa mpaka sasa wamebaini kuwepo kwa maambukizi mapya zaidi ya 759 kwenye ukanda huo hali inayoogofya kuhusu kuendelea kusambaa kwa virusi hivyo.

Idadi hii mpya inafanya kufikia kiwango cha asilimia 38 cha maambukizi mpaya ukilinganisha na kiwango cha asilimia 27 mwezi April mwaka huu wakati shirika la Afya duniani lilipotoa takwimu za mwisho kuonesha mwenendo wa ugonjwa huo ambao ulionekana kana kwamba umedhibitiwa.

Takwimu hizi zimetolewa wakati wa mkutano unaowakutanisha mawaziri wa afya toka mataifa kumi na moja ya ukanda wa Afrika Magharibi, mkutano unaofanyika nchini Ghana ukilenga kutafuta mbinu mpya za kukabiliana na maambukizi zaidi ya virusi vya Ebola.

Virusi vya Ugonjwa wa Ebola huweza kuambukizwa kwa njia ya hewa na kugusana hii ni kwa mujibu wa ripoti ya WHO, ambapo umetajwa kuwa miongoni mwa magonjwa hatari zaidi duniani, ugonjwa ambao mpaka sasa haujapatiwa tiba.

Mtu aupatapo ugonjwa huu huweza kuwa na homa kali, maumivu ya viungo, kutapika na kuhara na wakati mwingine kushindwa kufanya kazi kwa baadhi ya ogani za mwili na kutokwa damu mfululizo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...