Mahakama
nchini Afrika kusini imerefusha muda wa kutathmini ombi la Serikali
ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo la kurejeshwa nyumbani kwa Pasta
Joseph Mukungubila anaye tuhumiwa kupanga njama za kuipinduwa
serikali ya nchi hiyo mwaka uliopita.
Uamuzi huo umechukuliwa na jaji wa mahakama ya mjini Johanesbourg ambaye amesema uchunguzi wa ziada unaendelea zaidi, ambapo baadhi ya faili lililowasilisha na serikali ya DRCongo halikuheshimu sheria na taratibu.

Mukungubila mwenyewe alikuwepo mahakamani hapo wakati uamuzi huo unachukuliwa akiwa na baadhi ya watu wa karibu yake ambao waliandamana dhidi ya rais Joseph Kabila.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire