Antonio Guterres, mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na wakimbizi UNHCR |
Zaidi
ya wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni moja barani Afrika,
wanakabiliwa na baa la njaa wakati huu mashirika ya misaada ya
kimataifa yakiendelea kukabiliana na changamoto ya kupata chakula cha
msaada, Umoja wa Mataifa umesema.
Idadi
hii imeongezeka kutokana na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile
UNHCR na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kuanza kusitisha na
kupunguza ugawaji wa chakula cha kila siku kwa maelefu ya wakimbizi
duniani kutokana na kukabiliwa na uhaba wa chakula.
Mashirika
haya yanasema kuwa ili kunusu hali kuwa mbaya zaidi yanahitaji kupata
kiasi cha dola za Marekani milioni 225 ili kuwawezesha kupata chakula
cha kila siku kwa wakimbizi na kuondoa kabisa mpango wao wa kupunguza
ugawaji wa chakula.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire