Watu
saba wauawa wakiwemo askari polisi 4 baada ya watu wenye silaha
kushambulia gari ya abiria katika pwani ya kenya eneo la Lamu.
Washambuliaji
walifyatulia risasi gari hilo jirani na mji wa Witu takribani
kilomita 50 kutoka kisiwa cha lamu.
Baada
ya shambulizi hilo waliwakabili polisi waliowasili katika eneo hilo
kuokoa na tayari kundi la wapiganaji wa al shabab limekiri kutekeleza
mauaji hayo.
Takribani
watu mia moja wameuawa katika ghasia huko Pwani nchini kenya katika
msimu huu huku raia wakiyakimbia makazi yao na sekta ya utalii wa
ndani kuzorota.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire