ulinzi
na usalama vimeimarishwa vya kutosha kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Antebbe nchini Uganda baada ya kuwepo kwa taarifa za kutokea kwa shambulio la kigaidi.
Kitisho
hicho kimetolewa wakati huu viwanja vya ndege vya ulaya na mashariki
ya kati vikiimarisha usalama zaidi baada ya Marekani kuarifu kuhusu
kitisho cha kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi.
Ubalozi
wa Marekani jijini Kampala ulipewa taarifa na polisi nchini Uganda
juu ya uwepo wa mpango wa kutokea kwa shambulio la Kigaidi hapo jana
usiku saa tatu usiku hadi saa tano kwenye uwanja wa ndege wa Antebbe
na kundi lisilojulikana.
Hakuna
tukio liliripotiwa hadi sasa. Hata hivyo Hakuna jina lolote
lililotajwa la kundi ambalo linalotishia kuendesha mashambulizi.
Wanamgambo wa Al Shabab, hivi karibuni walikiri kuhusika katika
mashambulio nchini Kenya , Djibouti na Somalia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire