Maaskofu
wa makanisa mbalimbali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameyatuhumu
makundi ya Seleka na Anti-Balaka kuwa chanzo cha kuendelea kuzorota
kwa hali ya usalama kwenye taifa hilo ambalo linakabiliwa na
changamoto za kiusalama kufuatia mauaji ya kidini.
Viongozi
hao wa kidini wanadai kuwa makundi kama vile ya Seleka, Anti-Balaka,
na kundi la LRA la nchini Uganda yamekuwa yakijichukulia sheria
mkononi kwa kutekeleza mauaji dhidi ya raia wanaowakamata.
Licha
ya sehemu kubwa ya mauaji ya kudhibitiwa mjini Bangui, bado maeneo
mengine ya nchi yemeendelea kushuhudia uwepo wa matukio ya
unyanyasaji, mateso na mauji dhidi ya raia yanayofanywa na makundi
haya, ambapo viongozi wa dini sasa wanataka makundi hayo kukomesha
vitendo vya kikatili.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire