Pages

mardi 11 février 2014

UPINZANI NA SERIKALI YA SYRIA WAENDELEA KUVUTANA KATIKA MAZUNGUMZO YA GENEVA USWISI

Wajumbe wa upinzani nchini Syria wanaoshiriki katika mazungumzo ya Geneva wameonya kuwa hawatarejea tena katika mazungumzo kama hakutakuwa na hatua itakayopigwa katik mazungumzo yanayoendelea sasa.

Wajumbe hao wamesema kuwa kutokuwepo kwa maendeleo katika mazungumzo hayo ni sawa na kupoteza muda kauli ambayo wamaeitoa mbele ya mjumbe wa usuluhishi wa umoja wa mataifa na nchi za kiarabu Lahkdar Brahimi.
Hayo yanakuja huku pande hizo mbili zikiendea kuvutana na kutupiana lawama kuhusu hatua ya kushambuliwa kwa wafanyakazi wa misaada wa umoja wa mataifa hivi karibuni mjini Homs.
Upinzani kwa upande wake unatupa lawama kwa majeshi ya serikali ya Bashar Al Assad kuwa ndiyo yalifanya mashambulizi hayo.

Kwa upande wake Serikali ya Syria imesema kuwa iko tayari kwa majadiliano yoyote ambayo yatasaidia kumaliza mgogoro wa nchi hiyo. 


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...