Mkuu
wa shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa Valerie Amos
amelitaka Baraza la Usalama la umoja huo kuchukua hatua za haraka
kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika kwa wakati kwenye maeneo
yaliyoathiriwa na mapigano.
Valeria
Amos amesema haikubaliki kuona serikali ya Damascus na makundi ya
waasi yanaendelea kukika sheria kwa kukwamisha ufikishwaji wa misaada
ya kibinadamu, huku akikiri kuwa changamoto bado ni katika zoezi
hilo.
Wakati
huo huo majadiliani baina ya wajumbe wa serikali ya Damascus na
wapinzani yameendelea mjini Ganeva Uswisi, pande zote zimeendelea
kutofautiana juu ya ajenda za mazungumzo.
Mpatanishi
wa mgogoro huo Lakhdar Brahimi amesema mazungumzo hayo bado yana
changamoto kubwa na itakuwa vigumu kusonga mbele bila kuafikiana.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire