Pages

mercredi 19 février 2014

MCHEZAJI WA KIMATAIFA RAIA WA UFARANSA OLIVIER GIROUD AKANA KWENDA NJE YA NDOA

 Mchezaji wa kimataifa raia wa Ufaransa Olivier Giroud amekanusha madai kwamba amejihusisha na mapenzi nje ya ndoa.

Baada ya kuomba radhi hadharani kufuatia gazeti moja nchini Uingereza kubaini kuwa mchezaji huyo ametoka kimapenzi na msichana mmoja.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter mshambuliaji huyo wa Arsenal amekiri kufanya kosa huku akisisitiza kwamba hajafanya mapenzi kinyume ya ndoa, Giroud amesema"Nikweli nimefanya kosa lakini sijafanya mapenzi nje ya ndoa yangu, inabidi mambo yawe wazi"

gazeti la The Sun liliandika kuwa Giroud mwenye umri wa miaka 27, ambaye ni baba wa familia alimuita mwanamitindo mmoja katika Hoteli ambako walikuwa wamepiga kambni wachezaji wa the Gunners siku moja kabla ya mechi yao na Cristal Palace ambapo walishinda mabao 2 kwa 0 Februari 2 mwaka huu wa 2014.

baada gazeti hilo lilichapisha picha ya mcehzaji huyo akiwa amevalia chupi, picha ambayo alipigwa na msichana huyo ambaye alikiri kuwa hajafanya mapenzi na mchdzaji huyo.




Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...