Riek Machar kushoto na Salva Kiir maswaiba wa zamani ambao leo ni mahasimu |
Waasi
wanamtii makama rais wa zamani wa Sudani Kusini pamoja na majeshi ya
serikali ya rais Salva Kiir yanatuhumiwa kutekeleza mauaji ya kivita
katika vita vya kuiteka miji kadhaa nchini humo tangu Desemba 15
mwaka jana.
Kwa
mujibu wa Ripoti ya Umoja wa mataifa vitendo vya ukiukwaji wa haki za
binadamu vimetekelezwa na pande zote mbili nchini Sudani Kusini
ambapo hivio karibuni wanawake na watoto wamebakwa wakiwa Hospitalini
na kuuawa, huku wakimbizi wakiuawa makanisani walikokimbilia.
duru
sahihi ambazo hazikupenda kutajwe kutokana na sababu za usalama,
zimearifu kuwa mjini Malakal kuna maiti nyingi ambazo ziliachwa
barabarani na ambazo zimekuwa zikiliwa na mbwa pamoja na ndege.
Siku
ya alhamisi juma lililopita siku mbili baada ya mji wa Malakal
kuanguka mikononi mwa waasi wanaomtii makama wa zamani wa rais Riek
Mashar, shirika la madaktari wasiokuw ana mipaka lilikuwa la kwanza
kuripoti kuhusu yaliojiri katika Hospitali ya chuo mjini hapo.
Wananchi
wengi walikimbilia katika vituo vya Umoja wa Mataifa ambavyo
vimepokea idadi kubwa ya watu waliokimbia makwao kufuatia usalama
mdogo.
Miongoni
mwa wakimbizi hao wanadai kuwa kumefanyika mauaji ya kikatili na
ubakaji wa wagonjwa katika Hospitali.
Duru
nyingine zimearifu kuwa wanawake wengi waliokuwa wamekwama katika
Hospital mjini Malakal wamebakwa na kuuawa. Waasi wanaomtii Riek
Mashar wanatuhumiwa kuwalenga watu wa kabila la rais Salva Kiir la
Dinka wakati majeshi ya serikali yakituhumiwa kuhusika katika mauaji
ya watu wakabila la Nuer.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire