Pages

mercredi 19 février 2014

MTOTO WA RAIS WA ZAMANI WA ZAMBIA ANDREW BANDA APINGA HUKUMU DHIDI YAKE NA ATAKATA RUFAA


Balozi na mtoto wa rais wa zamani wa Zambia, Rupia Banda, amesema atakata rufaa kwenye mahakama kuu nchini humo kupinga adhabu ya kifungo cha miaka mwili jela kwa makosa ya kupokea rushwa.

Andrew Banda ambaye mwishoni mwa juma lililopita mahakama mjini Lusaka ilimkuta na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi wakati akiwa balozi na kumuhukumu kifungo cha miaka 2 baada ya kuabinika kuwa alipokea rushwa toka kwa kampuni moja ya Italia ili kushinda tenda ya ujenzi wa barabara.

Wakili wa Andrew, Milner Katolo amesema mteja wake hivi sasa ameachiwa kwa dhamana ya kwacha elfu 10 sawa na dola za marekani elfu 1 na 700 wakati huu akisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake.

Andrew Banda ni miongoni mwa maofisa wa utawala uliopita ambao wamefunguliwa mashtaka ya rushwa kwenye kampeni iliyotangazwa na rais Michael Sata toka alipoingia madarakni mwaka 2011.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...