Pages

jeudi 13 février 2014

SHIRIKA LA UNESCO LAPONGEZA JUHUDI ZA RADIO WAKATI DUNIA IKIADHIMISHA SIKU YA RADIO


Dunia hii leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya Radio huku umoja wa mataifa ukisema kuwa bado kuna changamoto nyingi kuhusiana na usawa wa wanawake na wanaume katika vyombo vya utangazaji. Shirika la umoja wa mataifa la sayansi na utamaduni UNESCO limesema kuwa bado kuna kazi kubwa inayohitajika kufanywa ili kuhamasisha na kuleta usawa baina ya jinsia hizo mbili.

Hata hivyo UNESCO imenpongeza juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari, hasa Radio kwa kuunganisha jamii, kuhamasiha raia kuzingatia amani, maendeleo, haki za binadamu na mengineyo.

“Radio ni sauti inayokwenda mbali”, amesema Irina Bokova, mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya sayansi na utamaduni UNESCO.

Lakini mbali na hayo, amependekeza katika kuadhimisha siku hii ya kimataifa kuweko na jukumu la kumshirikisha mwananchi katika Radio, hasa akitoa mchango wake kwa manufaa ya kuendeleza jamii.

Irina Bokova, amepongeza mchango wa radio wakati nchi ya Haiti ilipokumbwa na majanga.

Kwa mujibu wa mkuu wa maendeleo ya vyombo vya habari na jamii wa UNESCO Mirta Lourenco, bado hakuna usawa katika vyombo hivyo vya utangazaji na mfumo dume unaendelea kutawala katika vyombo vingi.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire

KINACHOFANYWA NA RAIS NKURUNZIZA KWA SASA NDIO ULE MCHEZO WA NDANI?

Mkanganyiko umeendelea kushuhudiwa katika chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, chama ambacho hapo awali kilileta matumaini ya kuwau...