Kufuatia
saa kadhaa za majadiliano kati ya mawakili na maofisa wa uhamiaji wa
Afrika Kusini, hatimaye mahakama moja nchini Afrika Kusini,
imemruhusu Dk Paul Semugoma raia wa Uganda kuishi na kufanya kazi
nchini humo.
Juma
hili mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Johannesburg,
daktari huyo alizuiliwa kwa saa kadhaa na maofisa uhamiaji wa Afrika
Kusini wakitaka kumpandisha ndege na kumrudisha nchini mwake kufuatia
ombi la serikali ya Uganda.
Dk
Pauli Semugoma aliondoka nchini Uganda kuhofia maisha yake kufuatia
kuwa mstari wa mbele kuunga mkono ndoa za watu wa jinsia vitendo
ambavyo wabunge wa Uganda wamepitisha sheria kali kuzuia watu
kujihusisha na mapenzi ya aina hiyo.
Rais
wa Uganda Yoweri Museverni wakati wowote kuanzia sasa tatia saini
muswada huo na kuwa sheria ambapo mtu atakayepatikana na hatia
atakumbana na kifungo cha maisha jela.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire