Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, umeitolea wito serikali ya nchi hiyo juu ya heshima ya haki za upinzani,
wito ambao umekuja siku mbili baada ya kutokea matukio ya kumzuia kiongozi wa
upinzani Vital Kamerhe kusafiri kutoka Kinshasa kuelekea mjini Goma.
Katika taarifa iliotolewa na Umoja huo imesema wakati taifa hilo
likijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi wa madiwani, Mikoa, Wabunge na ule wa rais
mwaka 2016, ni muhimu kwa serikali ya rais Kabila kuheshimu haki ya kujitetea
haki ya upinzani na kutowa uhuru kwa wapinzani kutembelea maoeneo yote watakayo
Ujumbe huo wa Umoja wa Ulaya umesema unatiwa wasiwasi na hatuwa
ya serikali kuwazuia wapinzani kutembelea maeneo watakayo, na hivi karibuni ni
kuzuiliwa kwa rais wa chama cha UNC Vital Kamerehe ambaye amezuiliwa kuzuru mji
wa Goma.
Vital Kamerhe ambaye alichukuwa nafasi ya tatu katika uchaguzi mkuu uliopita, wa mwaka 2011 na ambao upinzani ulilalamika kugubikwa na udanganyifu, alijikuta akizuiliwa kusafiri kuelekea mjini Goma siku ya Ijumaa na Jumapili ambako alipanga kuanzisha mpango wa kuhamasisha amani katika eneo hilo lenye kukumbwa na machafuko.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire