Jenerali wa Majeshi ya Ufaransa katika Operseheni Sangaris nchini jamhuri ya Afrika ya Kati Francisco Soriano amewatahadharisha waasi wa kikristo wa kundi la Anti Balaka jijini Bangui ambao wamekuwa kikwazo cha kupatikana kwa amani nchini humo kwa kuendeleza mauaji dhidi ya waislam.
Katika mazungumzo yake na viongozi mbalimbali wa kidini hapo
jana jijini Bangui, jenerali Francisco
Soriano amesema anti Balaka wamekuwa maaduwi wa amani nchini Jamhuri ya Afrika
ya Kati.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian ambaye anafanya
ziara katika nchi kadhaa barani Afrika kuzungumzia juu ya mzozo wa jamhuri ya
Afrika kati amesema majeshi ya Ufaransa yataendelea kufanya kila jitihada
kuhakikisha Amani inarejea nchini humo.
Le Drian, anasubiriwa jijini Bangui hii leo ambapo itakuwa ni
ziara ya nne kufanywa na kiongozi huyo katika nchi hiyo tangu kuanza kwa
machafuko ya kidini yaliosababisha vifo vya maelfu ya watu huku wengine
wakilazimika kuyatoroka makwao.
Waziri
Le Drian amesema lengo la Operesheni Sangaris ni kuhakikisha usalama unarejea
na shughuli za kuwapokonya silaha wale wote wanaozimiliki kinyume cha sheria
zinafanyika bila kuegemea upande wowote, huku kipindi cha mpito kinaendelea ili
jamhuri ya Afrika ya kati iweze kupata amani ya kudumu.
Tahadhari hii ya jenerali Soriano inakuja siku moja baada ya kutokea mauaji ya
mbunge Jean Emmanuel Njaroua ambaye
aliuawa na watu wasiojulikana, ila wabunge wenzake wanawatuhumu waasi wa kundi
la Anti Balaka kuhusika na mauaji hayo.
Siku ya Jumamosi mbunge huyo alizungumza na ya wabunge na
kuonyesha dukuduku lake kuhusu mauaji yanayoendelea dhidi ya waumini wa kiislam
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire