Rais wa Marekani Barack Obama
amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Ufaransa katika
kusimamia upatikanaji wa amani na usalama wa dunia ikiwa ni pamoja na
kupambana na vitendo vya kigaidi. Rais Obama amesema Ufaransa chini ya
utawala wa Rais Francois Hollande imeonyesha ujasiri katika hatua za
kushughulikia migogoro inayozikumba nchi mbalimbali duniani.
Katika mkutano wa pamoja wa na vyombo vya habari, ma rais hao
wamepongezana kuhusu kudumisha mahusiano ya kihistoria wapofikia katika
ushirikiano licha ya kuwepo kwa mambo kadhaa ambayo yamekuwa
yakiwatofautisha.
Obama ameeleza kuwa ufaransa imejitoa kwa dhati kwenye migogoro ya
nchi za Syria, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati na changamoto
inayotokana na mpango wa nyuklia wa nchi ya Iran amabayo imekuwa katika
mvutano mkali na mataifa yenye nguvu duniani.
Katika hatua nyingine rais huyo wa marekani amesema kuwa Marekani
itaendelea kuwa na ushirikiano mzuri na nchi za ulaya bila kubagua kwa
kuwa nchi zote ni muhimu.
Kwa upande wake rais Francois Hollande amesema kuwa Ufaransa
itaendelea kutoa ushirikiano kwa Marekani ili kushughulikia masuala
yanayohusu amani, usalama na vita dhidi ya vitendo vya kigaidi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire