Kiongozi
wa majeshi ya katika Ikulu ya rais nchini Mali jenerali Yamousa
Camara ametiwa nguvuni jana baada ya kuhusishwa katika mauaji ya
wanajeshi wa kofia nyekundu wafuasi wa rais wa zamani wa nchi hiyo
Amadou Tounai Toure ATT. Miili ya wanajeshi 21 iliokotwa desemba 4
mwaka jana katika shimo la pamoja karibu na jiji la bamako
Duru za kishiria nchini Mali zimearifu kuwa Jenerali Camara ambaye ni waziri wa zamani wa ulinzi ametiwa nguvuni baada ya kuhusishwa na mauaji ya wanajeshi hao wa serikali ya zamani waliokutwa katika shimo la pamoja miezi mitano iliopita.
Wanaharakati
wa kutetea haki za wanajeshi hao wamesema hii ni hatuwa ya kwanza na
ukweli lazima uwekwe wazi juu ya mauaji hayo.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire