Mahakama
ya Uhalifu wa kivita ya ICC ambayo ilikutana jana ili kutowa uamuzi
iwapo kiongozi wa zamani wa kivita mashariki mwa DRCongo Bosco
Ntaganda ana kesi ya kujibu, na kumkuta na hatia ya kuhusika katika
mauji ya kikabila kati ya mwaka 2002-2003 pamoja pia na ubakaji wa
watoto.
Akizungumza
mbele ya mahakama, muendesha mashataka mkuu wa ICC Fatou Bensouda
amethibitisha kuwa Ntaganda anahusika na mauji ya kivita kufuatia
ushuhuda wa binti mmoja alieingizwa jeshini na ambaye alibakwa mara
kadhaa na wanajeshi wa Ntaganda wakati akipewa mafunzo.
Ajouter une légende |
Ntaganda
ambaye alipewa jina la Terminator kufuatia ukatili wake na kutokuwa
na huruma ana tuhumiwa pia kutekeleza ubakaji na kufanya watumwa wa
ngono wasichana wenye umri wa chini ya miaka 15. Fatou Bensouda ni
muendesha mashtaka mkuu wa ICC.
Hata
hivyo, upande wa utetezi unaendelea kusisitiza kuwa kiongozi huyo wa
zamani wa waasi wa UPC hakuwa na maslahi yoyote kutekeleza mauwaji
hayo kwa vile yeye sio wa kabila la Walema au walendu.
Ntaganda
alijisalimisha mwenyewe mbele ya mahakama ya ICC March mwaka 2013
baada ya mambo kuwa mabaya kwake ambapo alikimbilia kwenye ubalozi wa
Marekani jijini Kigali nchini Rwanda kabla ya kupelekwa Hegue.
Ntganda
ana kesi ya kujibu dhidi ya Makosa ya kivita yaliotekelezwa na vikosi
vya kundi la FPLC ambavyo Ntaganda alikuwa kiongozi.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire