Hali ya sintofahamu yaebdelea kushuhudiwa jijini Bujumbura ambapo vyombo vya usalama vimezingira maeneo kadhaa ya jiji la Bujumbura.
kwa Mujibu wa msemaji wa jeshi Kanali Gaspard Baratuza, Kundi la watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito, wametekeleza mashambulizi mfululizo katika kambi mbili za jeshi jijini Bujumbura, Burundi, ambapo wapiganaji 12 wameuawa na wengine zaidi ya 24 wametiwa mbaroni, huku wanajeshi wa serikali wanaokadiriwa kufikia watano nao wakiuawa wakati wa makabiliano.
Mashambulizi
haya yakupangwa, ni mabaya zaidi kutekelezwa toka kulipofanyika
jaribio la mapinduzi lililoshindikana mwezi May mwaka huu.
Wapiganaji
hao walivamia kambi ya jeshi ya Nagara kaskazini mwa mji wa Bujumbura
pamoja na kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Iscam, kilichoko kusini
mwa nchi hiyo, baada ya kupora silaha katika kambi moja eneo hilo
mashambulizi yaliyoanzwa kutekelezwa alfajiri ya hii leo na kudumu
kwa zaidi ya saa nne
Kuliripotiwa
pia makabiliano ya risasi katika viunga kadhaa vya jiji la Bujumbura,
hali inayozidisha hofu ya kiusalama kwenye taifa hilo, wakati huu
ambapo inadaiwa kuwa rais Pierre Nkurunziza amefanya kikao cha
dharura na mawaziri wake kuizungumzia hali hiyo.
Shughuli
zimesimama jijini Bujumbura, hakuna mawasiliano ya watu kutoka katika
mtaa mmoja kuelekea mtaa mwingine, hali ambayo inalalamikwa na
wananchi wa kaazi wa jiji la Bujumbura baada ya kukosa chakula
kutokana na kuzuiliwa kwa barabara zote kuu
Polisi
na wanajeshi nchini Burundi, wanasema wanaendelea na uchunguzi
kuhusiana na tukio hili pamoja na kuendesha msako wa wapiganaji zaidi
walioripotiwa kukimbia baada ya mashambulizi haya.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire