Maelfu
ya mashabiki wamejitokeza huko Mumbai kwa ajili ya mazishi ya Sridevi
Kapoor, muigizaji nyota wa filamu za Bollywood ambaye alipata ajali
ya kuzama bafuni katika hoteli moja huko Dubai mwishoni mwa juma
lililopita ambako alikuwa amekwenda kuhudhuria sherehe ya harusi ya
mwipwa wake.
Makundi
ya watu wamejitokeza jana Jumatano asubuhi ili kutoa kuheshimu zao za
mwisho kwa muigizaji huyo nyota wa filamu mwenye umri wa miaka 54
kabla ya kufanyika kwa mazishi yake
Mwili
wake uliwekwa kwenye kikapu cha kioo kilichofunikwa na bendera ya
India wakati akipelekwa katika safari yake ya mwisho kwenda kwenye
chumba cha kuchomwa moto huku mumewe Boney Kapoor akisimama karibu.
Siku
ya Jumapili asubuhi, familia ya muigizaji huyo ilithibitisha kifo
chake ambapo polisi nchini India ilizuia muili kwa ajili ya
uchunguzi, na mwisho wa siku ikabainika kuwa aliza kwa ajali ndaniya
bafu.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire