Tume
inayofanya uchunguzi kuhusu matukio ya Desemba 31 mwaka 2017 na
Januari 22 mwaka 2018 wakati wa maandamano nchini DRCongo, imesema
jumla watu 14 walipoteza maisha 7 ikiwa ni wakati wa maandamano
yaliotishwa na kanisa katoliki kupinga utawala wa rais Joseph Kabila.
Takwimu hizo zimetolewa Jumamosi March 10 na waziri wa haki za binadamu
nchini DRCongo Marie Ange Mushobekwa alieambatana na ripota wa tume
hiyo Georges Kapiamba ambae anawakilisha mashirika ya kiraia na
kukubaliana kuhusu takwimu hiyo.
Takriban
Waathirika na mashuhuda 122 walikubali kujibu wito uliotolewa na tume
ambapo watu 14 waliuawa, 12 kwa risase na wengine 2 kwa moshi wa bomu
za kutoa machozi huku wengine 65 wakijeruhiwa na wengi kwa risase.
Wakati
huo huo tume hiyo imesema watu zaidi 40 walikamatwa na kufanyiwa
vitendo vya unyanyasaji katika matukio ya Desemba 31 mwaka 2017 na
januari 21 mwaka 2018.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire