Chama
tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD mwishoni mwa juma kimemtangaza
rais Pierre Nkurunziza kuwa kiongozi wa juu wa chama, hatua
inayomfanya awe kiongozi wa maisha katika mkutano wa viongozi wa juu uliofanyika katika tarafa ya Buye anakotoka rais huyo.
Licha
ya taarifa ya chama hicho iliyotolewa mwishoni mwa juma kutoeleza kwa
kina kuhusu nafasi mpya waliyompa Nkurunziza, lakini ni wazi sasa
kiongozi huyo anafanywa kuwa mtawala wa maisha, hatua inayozidisha
sintofahamu zaidi kwenye siasa za nchi hiyo.
Haijafahamika
ikiwa kutakuwa na marekebisho mengine ya katiba tofauti na yale
yanayotarajiwa kupigiwa kura mwezi Mei mwaka huu ambapo ikiwa
yataidhinishwa yatamruhusu kuwania urais kwenye uchaguzi wa mwaka
2020 na kumfanya abaki madarakani hadi mwaka 2034.
Hata hivyo kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusu hatuwa hiyo ambayo licha ya kuchukuliwa baadhi ya wafuasi wa chama wamenong'ona kuwa itakuwa ngumu kutekelezwa kwa hatuwa hiyo.
Chama hicho kimeahidi kutoa maelezo kuhusu cheo hicho na nini kitabadilika.
Evariste Ndayishimiye katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD amesema hakuna anaeweza kujifananisha na Pierre Nkurunziza katika chama hicho.
Wanasiasa wengi wa upinzani wamekosoa hatuwa hiyo ya chama tawala na kueleza kwamba kinataka kumfanya Nkurunziza kuwa kama Bokasa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire