Makundi
ya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamemuunga mkono
kiongozi aliye uhamishoni Moise Katumbi, hatua iliyofikiwa katika
mazungumzo yaliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Johannesburg,
Afrika Kusini.
Mazungumzo
haya ya mwishoni mwa juma yaliyowakutanisha wanasiasa wa upinzani
kutoka nchini DRC, yalilenga kuunda muungano utakaosimama kwenye
uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Katumbi
aliongoza mamia ya wanasiasa wa upinzani katika mkutano wa siku 3
jijini Johannesburg kutengeneza mkakati watakaoutumia wakati wa
uchaguzi mkuu wa Desemba 23 kuchukua nafasi ya rais Joseph Kabila
anaemaliza muda wake.
Wanasiasa
waliohudhuria mkutano huu wameonesha wazi kumuunga mkono gavana wa
zamani wa eneo la Katanga Moise Katumbi kusimama kama mgombea wa
muungano wa upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Katumbi
amesema anaamini muungano wao utakuwa silaha tosha ya kuleta
mabadiliko ya kidemokrasia nchini mwao, kauli ambayo imeonekana
kuungwa mkono na baadhi ya nchi za Ulaya zinazoshinikiza kufanyika
kwa uchaguzi wa mapema.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire