Takriban
watu 16 wameuawa kwa kupigwa na radi siku ya Jumamosi kusini mwa
Rwanda katika kanisa la wasabato, aifsaa mmoja wa eneo hilo ameeleza
hapo jana Jumapili.
Meya
wa Wilaya ya Nyaruguru Habitegeko Francois aliiambia shirika la
habari la Ufaransa AFP kupitia njia ya simu kwamba watu 14 walikufa
mara moja na wawili waliopoteza maisha baadae.
Watu
wengine 140 wamejeruhiwa na kupelekwa haraka hospitalini na vituo
vya afya, na madaktari wanasema watatu wao walikuwa katika hali mbaya
lakini sasa
wameanza kupata ahueni na wameruhisiwa kurejea nyumbani.
Kwa
mujibu wa taarifa
za meya,
tukio
kasma hilo lilitokea
Ijumaa katika eneo moja ambalo radi
ilipiga
kundi la wanafunzi 18, na kuua mmoja kati
yao.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire