Mbunge
wa chama cha KANU nchini Kenya Kassait Kamket, amependekeza mswada
bungeni unaolenga kubadilisha mfumo wa uongozi nchini humo kwa
kuibadilisha Katiba.
Mswada
huu iwapo utakubaliwa na wabunge, ina maana kuwa Katiba mpya ya Kenya
iliyopatikana mwaka 2010, itafanyiwa mabadiliko makubwa.
Mbunge
huyo anapendekeza kuundwa kwa wadhifa wa Waziri Mkuu atakayekuwa na
madaraka makubwa lakini pia kuwepo kwa rais ambaye atakuwa ishara ya
umoja wa kitaifa.
Iwapo
marekebisho hayo yatafanyika, bunge la pamoja, lile la kitaifa na
Senate litamchagua rais ambaye atakuwa na jukumu la kumteua Waziri
Mkuu kutoka kwenye chama chenye wabunge wengi bungeni.
Waziri
Mkuu atahudumu kwa muda wa miaka mitano kabla ya Uchaguzi mwingine
kufanyika, huku rais ambaye ni lazima awe na zaidi ya miaka 50,
akihudumu kwa muhula mmoja wa miaka saba.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire