Mwili
wa aliyekuwa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo CENI, padre Apolinaire Malu Malu Muholongu,
umewasili katika mji wa Butembo mkoani Kivu ya kaskazini ambako
unatarajiwa kuzikwa hivi leo.
Kabla
ya kusafirishwa hadi Butembo, mwili wa kiongozi huyo uliagwa na umati
wa watu mjini Kinshasa, wakiwemo wanasiasa na maaskofu wa kanisa
katoliki nchini DRC.
Katika
kuithamini kazi yake na juhudi nyingi za kidiplomasia alizoongoza kwa
niaba ya serikali ya nchi hiyo, Rais Joseph Kabila, amemtaja Malumalu
kama shujaa, akifananisha yale aliyoyafanya na viongozi maarufu
nchini humo kama, Emery Patrice Lumumba na marehemu Laurent Desire
Kabila.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire