Mashirika
sita ambayo yote yamesajiliwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na
nchi wananchama, juma hili yamewasilisha hoja kwa spika wa bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimtaka aitishe mkutano wa dharura wa
wabunge na kutoa tamko kuhusu machafuko yanyoendelea kushuhudiwa
nchini Burundi.
Mashirika
hayo, yanatoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti na za haraka
kushughulikia mzozo wa kisiasa na hali ya kibinadamu nchini Burundi,
wakati huu mashirika hayo yakidai kuwa hali imezidi kuwa mbaya kwenye
taifa hilo hukuviongozi wa Burundi wakikaidi maazimio kadhaa ya wakuu
wa nchi za Afrika mashariki na Umoja wa Afrika.
Katika
hoja yao, mashirika hayo yanataka kuwekewa vikwazo kwa viongozi wa
Burundi, kupelekwa kwa waangalizi wa kimataifa pamoja na wanajeshi wa
Umoja wa Afrika watakaolinda usalama wa raia.
Spika
wa bunge la Afrika Mashariki, Dan Kidega amepokea hoja ya mashirika
hayo, na kusema kuwa imekuja wakati muafaka kwakuwa hali
inayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi, haiwezi kuendelea kutazamwa
bila ya kuchukuliwa hatua.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire