Ikiwa
hii leo ndio kilele cha mkutano wa kimataifa kati ya viongozi wa bara
la Afrika na Marekani, tayari mkutano huo umeza matunda ambapo rais
Barack Obama ametangaza uwekezaji wa nchi yake barani Afrika
unaofikia kiasi cha dola bilioni 33.
Rais
Obama amesema kuwa wafanyabiashara nchi humo wametenga kiasi cha dola
bilioni 14 kwenye uwekezaji wa maeneo tofauti huku kiasi kingine cha
bilioni 12 kikitengwa kwaajili ya uwekezaji kwenye sekta ya nishati.
Akiwahutubia
wajumbe wa mkutano huo, rais wa zamani wa Marekani Billy Clinton
amesisitiza nchi ya Marekani kuwa rafiki wa karibu wa bara la Afrika
kwenye shughuli za kimaendeleo na kwamba siku za usoni bara hilo
litakuwa linategemewa na dunia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire