Serikali
ya Washington imeonya kuwa waasi wa zamani wa kihutu kutoka Rwanda
waliopiga kambi mashariki mwa DRCongo wa FDLR lazima wajisalimishe
ili kuepuka kuchukuliwa hatuwa za kijeshi zenye lengo la
kulisambaratisha kundi hilo.
Mjumbe
maalum wa Marekani katika Ukanda wa maziwa makuu Russ Feingold
amefahamisha kuwa viongozi wa nchi za ukanda wa maziwa makuu
watakutana kwenye Umoja wa Mataifa siku ya alhamisi ili kujadili
kuhusu hatuwa za kuchukuwa dhidi ya kundi la FDLR.
Kiongozi
huyo amesema waasi hao wa zamani wanatakiwa kijisalimisha kwa wingi
la sivyo hatuwa za kijeshi zitachukuliwa. Feingold anaona kuwa hakuna
sababu zozote za kundi hilo kutaka majadiliano ya kisiasa na kundi
hilo lazima livunjwe kabla ya mwisho w mwaka huu wa 2014.
wapiganaji
takriban 200 wa kundi hilo walijisalmisha mwezi Mei, kwa sasa
mchakato huo ambao ulitakiwa kuendelea lakini sasa umesimama.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire