Nchi za Afrika Magharibi
zimetangaza hali ya hatari kwa kuzidiwa na idadi ya vifo kutokana na
Ugonjwa wa Ebola ambapo watu wapatao elfu moja sasa wanaripotiwa kufa
kwa maambukizi ya virusi hivyo.
Hali hiyo imetangazwa wakati
Bunge la nchi ya Liberia limekutana kwa dharura kupitisha sheria ya
kuweka vizuwizi vya barabarani na kikomo cha usafiri kwa watu
wanaoelekea mji mkuu wa Monrovia nchini humo na kuridhia siku 90 ya
hali ya hatari.
Aidha, miji miwili mashariki
mwa nchi ya Sierra Leone, Kailahun na Kenema, imewekwa chini ya hali
ya tahadhari kufwatia kauli ya msemaji wa serikali siku ya Alhamis
kuamuru shughuli za vilabu vya usiku na sehemu za burudani na starehe
kufungwa.
Madaktari wa sekta ya umma nchini Nigeria kwa upande wao wamesitisha mgomo wao wa mwezi mmoja kwa hofu ya ongezeko la maambukizi katika nchi ambayo ni ya kwanza barani Afrika kwa idadi ya wakazi wake na ambapo vifo vya watu wawili na maambukizi ya watu watano vimeripotiwa mjini Lagos.
Wakati hayo yakijiri, Shirika
la Afya duniani WHO linatarajiwa hii leo kujadili ikiwa litatangaza
hali ya "hatari ya afya kimataifa" katika mkutano wake wa
dharura mjini Geneva- Uswisi, pamoja na hatua mpya ikiwa ni pamoja
na vikwazo vya kusafiri kimataifa, hasa baada ya serikali ya
Uhispania kutuma helikopta ya kijeshi kumrejesha nchini humo daktari
Juliana Bonoha Bohe ambaye alifanya kazi katika hospitali moja mjini
Monrovia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire