Wanadiplomasia wa Umoja wa
Ulaya walioko mjini Kinshasa- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
wameelezea wasiwasi wao baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani
Jean Bertrand Ewanga, Mbunge na Katibu mkuu wa chama cha upinzani
cha UNC cha bwana Vital Kamerhe siku ya Jumanne tarehe 5 mwezi Agosti
mwaka huu.
Mabalozi hao, Luc Hallade wa
Ufaransa, Michel Latshenko wa Ubelgiji, na Naibu Balozi wa
Uingereza, John Lamb, kwa pamoja wamebaini wasiwasi wao kwa spika wa
Bunge nchini DRC Aubin Minaku na kutoa wito kwa serikali ya Congo
kuchukua hatua mahususi ili kutowa uhuru na haki ya kujieleza
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire