Makamu
wa rais wa Kenya, William Ruto ameendelea kusisitiza msimamo wa
Serikali ya nchi hiyo kuhusu hatua waliyoitangaza juma moja
lililopita ya kuwapokonya ardhi watu binafsi na makampuni yanayodaiwa
kunyakua ardhi kwa nguvu kwenye mji wa Lamu pwania ya Kenya.
Kauli
ya makamu wa rais, Ruto ameitoa akijibu hoja zinazotolewa na upinzani
ambao unataka Serikali kuachana na mpango huo na kwamba utachukua
hatua za kisheria kupinga uamuzi wa Serikali, msimamo ambao naibu wa
rais Ruto anasema serikali yake haitorudi nyuma wala kutishika.
Makamu
wa rais William Ruto anasema kuwa ni kitendo cha kustaajabisha na
kilichopitwa na wakati kuona viongozi wa upinzani wanatumia muda
mwingi kutoa vitisho dhidi ya Serikali na kuongeza kuwa vitisho hivi
havisaidii.
Makamu
wa rais Ruto, aanatoa kauli hii wakati ambapo hii leo tume ya ardhi
nchini humo inatarajiwa kuanza kutekeleza agizo la rais Uhuru
Kenyatta kuchukua ardhi inayokadiriwa kufikia hekari laki 5ambayo
ilikuwa inamilikiwa kinyume cha sheria.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire