Saa
chache baada ya kujiuzulu kwa mmoja wa mawaziri kwenye ofisi ya
wizara ya mambo ya nje ya Uingereza na mwanamke wa kwanza muislamu
kushika wadhifa huo, uamuzi wake umekosolewa na baadhi ya mawaziri
wenzake.
Baroness
Sayeeda Warsi waziri aliyekuwa akihusika na masuala ya imani na jamii
kwenye serikali ya waziri mkuu David Cameroon, ametangaza uamuzi wake
katika kile alichodai ni sera mbovu ya nchi hiyo kuhusu eneo la
mashariki ya kati na has mzozo kati ya Israel na Palestina.
Umuzi
wake umekosolewa vikali na waziri anayehusika na masuala ya hazina
nchini humo George Osbone ambaye anaona kuwa umuzi wa haukuwa sahihi
wala haukuwa na mantiki kwakuwa suala la mzozo wa Palestina lilikuwa
linashughulikiwa kidiplomasia.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire