Waasi wa Kihutu waliopiga kambi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa FDLR wamekataa kuondoka katika kambi ya Kanyabayonga iliotengwsa kuwakusanya kuelekea mjini Kisangani.
Mashirika ya
kiraia na shirika la Umoja wa Mataifa nchini DRCongo yamesema kuguswa
sana hatuwa hiyo ya wapiganani hao wa FDLR ambao wanatakiwa
kuondolewa katika maeneo ya kivu kaskazini na na Kivu Kusini na
kuepelekwa mjini Kisangani kabla ya kuondolewa katika ardhi ya
DRCongo.
waasi hao
wanasema hawakuwa na taarifa ya kuondoka wakati tayari Umoja wa
Mtaifa nchini DRCongo ulikuwa umetenga malori yatayo wasafirisha
kuelekea kisangani wakati ambapo Umoja wa Mataifa unasema tangu
mapema taarifa ya kuondoka kuelekea Kisangani inafahamika kitambo.
Hata hivyo
katribu mtendani wa kundi hilo la FDLR Wilson Irategeka amesema
wananchi wa aKisangani na mashrika ya kiraia ndio yamekataa kuwaona
mjini Kisangani, jambo ambalo limekanushwa na mwenyekiti wa mashirika
ya kiraia katika Mkoa wa Kivu Thomas d'Aquin.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire